Winga wa Ajabu Atua Dar

AL AHLY ya Misri inakuja Dar es Salaam wikichache zijazo na mchezaji wa ajabu. Kwa lugha za mtaani unaeza kusema ni mchezaji wa kufuru. Yaani gharama yake inasajili vikosi vyote vya Ligi Kuu Bara na chenji inabaki. Kikosi kizima cha Simba ni Sh 1.3 Bilioni.

 

Yaani hapo unajumuisha watu kama Cletus Chama,Emmanuel Okwi, John Bocco, Meddie Kagere, Jonas Mkude, Aishi Manula. Usisahau kina Erasto Nyoni, James Kotei, Said Ndemla, Shiza Kichuya, Adam Saramba,Paschal Wawa, Shomari Kapombe na wengine kibaoo… ambao wanatamba Msimbazi.

 

Sasa Al Ahly ya Misri ambayo ipo kundi moja na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika imesajili winga matata Hussein El-Shahat kutoka Al Ain ya Falme za Kiarabu (UAE)kwa thamani ya Sh11.5 Bilioni. Piga hesabu hapo uone anaingia mara ngapi katika kikosi cha Simba, haipungui mara 10 tena na chenji inabaki nyingi tu.

 

Ndiye mchezaji ghali zaidi klabuni hapo na imemsajili kutoka kwenye klabu ya Ain ya Falme za Kiarabu. Mchezaji huyo ni raia wa Misri ambaye amecheza soka la kulipwa miaka mingi.

 

Ahly ambao lengo la kuhakikisha wanafanya maajabu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, wameshamalizana na mchezaji huyo mwenye miaka 26 ambaye Ligi Kuu ya UAE alipachika mabao 15 msimu huu na kutoa asisti 17 katika michezo 33 ya mashindano yote.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment