The House of Favourite Newspapers

RC MWANZA AAMURU WALIOIBA MITIHANI WAKAMATWE – VIDEO

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Jonathan Shanna, kuwakamata mara moja na kuwatia ndani walimu wote na viongozi waliotajwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kuwa wamehusika na wizi wa mtihani ya kumaliza elimu ya msingi mkoani humo.

 

Mongella ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, Oktoba 6, 2018 alipokutana na walimu wa shule za msingi na sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza  na idara ya elimu ya mkoa huo ili kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu wa mitihani.

 

“Huu wizi wa mtihani ni mikakati ya muda mrefu, hapa Mwanza Jiji ndiyo vinara wa wizi huu, mwaka jana ilikuwa hivihivi Alliance wakati wa mtihani wa foRm six, na kituo hiki kimefungwa, leo wameongezeka New Alliance na Kisiwani, hapo inaonekana kuna mfumo umejikita wa wizi wa mitihani.

 

“Taarifa tulizo nazo ni kwamba mitihani ikifika kabla haijafunguliwa, kuna walimu, wakuu wa shule, wamiliki wa shule nadhan,i hata kwenye idara zetu za elimu wapo wanahusika kuiba. Ninataka wote walioelekezwa kuondolewa kwenye nafasi hizo wakisubiri mamlaka zao kufanya maamuzi, kufikia leo saa sita maamuzi yawe yamefanyika.

 

“Mkurugenzi wa Jiji Mwanza, Buchosa na wa Kwimba kama watakuwa hajafanya maamuzi tutawafanyia maamuzi wao. Wahusika waadhibiwe kama inavyopaswa. TAKUKURU na polisi kamateni hao watu, RPC hii biashara ni ya leo, kamateni wote, mamlaka zao zitawakuta Polisi Butimba,” alisema Mongella.

 

VIDEO: MSIKIE MONGELLA AKIFUNGUKA

Comments are closed.