The House of Favourite Newspapers

Wizkid, Tiwa Savage Wapata Dili Nono Kimataifa

WASANII maarufu kutoka Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun ‘Starboy Wizkid’ na Tiwa Savage wamepata nafasi ya kushiriki katika Ep ya ‘Global Citizen’ kutoka kwa kundi kubwa duniani, ‘Coldplay’ ambalo linafanya muziki aina ya Rock.

 

Mastaa wakubwa watakaokuwa ndani ya Ep hiyo ni Danny Ocean, David Guetta, Cassper Nyovest toka South Africa, Los Unidades, Pharrell Williams  na Nelson Mandela.

 

Wizkid na Tiwa Savage watakuwa kwenye wimbo mmoja na Star ‘David Guetta’ kwenye wimbo unaoitwa ‘Voodoo’ ambao ni wa mwisho kwenye Ep hiyo.

 

Global Citizen EP inategemewa kuingia sokoni siku ya Ijumaa, November 30 mwaka huu.

NYIMBO ZITAKAZOPATIKANA KWENYE E

1:“Rise Up” (feat. Nelson Mandela) – Stargate

2: “E-Lo” (feat. Jozzy) – Los Unidades and Pharrell Williams

3: “Timbuktu” (feat. Stormzy & Jess Kent) – Cassper Nyovest and Los Unidades

4: “Voodoo” (feat. Tiwa Savage, Wizkid, Danny Ocean & David Guetta) – Stargate and Los Unidades

Comments are closed.