The House of Favourite Newspapers

Wolper Afunga Mdomo Ishu Ya Kusalitiwa

Jacqueline Wolper

BAADA ya picha za mpenzi wa Jacqueline Wolper anayejulikana kwa jina la Brown zinazomuonesha akiwa kimahaba na mwanamke mwingine kuzagaa mitandaoni kitendo kinachoonesha kuwa ni usaliti, msanii huyo amepata kigugumizi na kushindwa kuelezea kama wameachana au vipi.

 

Risasi Jumamosi lilipozinyaka picha hizo lilimtafuta Wolper na kumuuliza kinachoendelea kati yake na mpenzi wake huyo kama wameachana au la kwani hata yeye alitupia video inayomuonesha akiimba kwa hisia kali huku macho yakionekana kuwa amelia sana lakini alipata kigugumizi na kudai kwamba hajaziona hizo picha labda atumiwe na alipotumiwa hakujibu chochote.

 

“Jamani hizo picha sijaziona hebu nitumie nizione halafu unipigie simu nitakujibu,” alisema Wolper lakini alipotumiwa kwa njia ya WhatsApp hakujibu chochote na alipoonana na paparazi wetu alisema hawezi kuzungumza chochote kuhusiana na uhusiano wake.

Stori: Gladness Mallya | Risasi Jumamosi.

Nuh Mziwanda Noma Aijibu Ndoa Ya Shilole

 

LIVE: Makeke ya JWTZ Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania

Comments are closed.