The House of Favourite Newspapers

Wolper awalipua Wadosi wanaowanyonya

0

wolperNa Mwandishi Wetu

Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amewatolea uvivu baadhi ya Wadosi wanaosambaza  filamu zao akidai kuwa wamekuwa hawawatendei haki kwani wanawanyonya kupitia kazi zao.

Akizungumzia jinsi wasanii wananyonufaika na kazi zao, Wolper alisema kuwa, wamekuwa wakifanya kazi nyingi na zinazofanya vizuri sokoni lakini cha ajabu wengi wa wasanii wana hali mbaya.

“Naomba niseme tu kwamba, hawa wadosi wanatunyonya sana, kuna wakati mimi niliandaa filamu yangu iliyonigharimu shilingi milioni 40 lakini nilipoipeleka kwa hao wasambazaji wa kidosi walinilipa shilingi milioni 25, unadhani katika mazingira hayo tutafika mbali?” alihoji Wolper.

Wolper aliongeza kuwa, licha ya kuonekana wana maisha mazuri, wengi pesa zao hawazipati kupitia filamu bali madili yao mengine na hiyo ni kuonesha jinsi wadosi waliokamata biashara hiyo wanavyowanyonya.

Leave A Reply