The House of Favourite Newspapers

Wolper: Instagram Inavunja Ndoa Kweupe

0

JACQUELINE Wolper ambaye siku hizi wanamuita Mama P; ni mwanamama mjasiriamali wa Bongo Movies ambaye amevunja ukimya juu ya uwezekano wa watu wa Instagram kuvunja ndoa ya mtu mchana kweupe.

 

Wolper anasema; “Hivi sasa unaweza kuamka asubuhi kumekucha au mchana kweupe ukashangaa watu wa Instagram wamevunja ndoa yako bila kutarajia ghafla tu.

 

“Mimi sijui nitoe ushauri gani, lakini kuna vitu kama video za kuunganisha zinaumiza sana familia za watu, naomba tuache kidogo au tupunguze ili ndoa zidumu…”

 

Kauli hii ya Wolper inakuja wakati huu ambapo kuna mambo mengi yanazungumzwa kutokana na Wimbo wa Nawaza wa Diamond Platnumz ambao umeibua mambo mengi, miongoni mwayo ni tetesi za kutibua ndoa ya Lulu.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply