The House of Favourite Newspapers

Wydad yatuma makachero kuifuatilia Simba Kwa Mkapa

0

Taarifa kutoka Morocco zinasema kuwa, Klabu ya soka ya Wydad Athletic itatuma wawakilishi nchini Tanzania ili kufuatilia kwa karibu mchezo kati ya Simba na Jwaneng Galaxy.

Wydad wana matumaini wanaweza kupata ushindi dhidi ya ASEC na wanatumai Galaxy inaweza kusababisha taharuki jijini Dar es Salaam. Wydad wanaamini wataifunga ASEC na wanatumaini Galaxy wataifunga Simba.

Dhumuni la Wydad kuleta watu nchini Tanzania ni kwa ajili ya kufanya uchunguzi kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Jwaneng ili kuangalia kama Simba na Jwaneng watasaidiana kupanga matokeo, ili waweze kupeleka malalamiko CAF

Msimu huu Simba kwenye mashindano ya CAF Champions League imecheza michezo saba (7) ameshinda mchezo mmoja pekee na Wydad Casablanca, amefungwa mmoja na ametoka sare mitano (5).

Leave A Reply