The House of Favourite Newspapers

Yafahamu Maajabu Matano Katika Mwili wa Binadamu

 Nywele nyekundu
Watu wenye nywele nyekundu duniani (watu weupe, Wazungu) ni wachache sana,wako chini ya asilimia mbili. Hivyo wana haki ya kufurahi na kujivuna.

Jicho linaloona rangi nyingi zaidi 
Watu wengi wana uwezo wa kuona rangi zipatazo milioni moja, japokuwa watu wenye upofu wa rangi huona rangi zipatazo  100,000 tu.  Kinyume chake, wenye uwezo mkubwa zaidi wa kuona rangi  (tetrachromacy) wanaweza kubaini rangi zipatazo milioni 99!

Nywele nyeupe
Pamoja na watoto wengi (weupe au wa Kizungu) kuzaliwa na nywele nyeupe, wengi wao nywele hizo hubadilika na kuwa nyeusi wanapokua.   Hivyo watu wazima wenye nywele nyeupe ni kati ya asilimia 2 na 16% tu.
Macho ya bluu
Ni asilimia 8 tu ya wanadamu wana macho ya blue.  Hali hii inayosababishwa na vinasaba hivi sasa imejitokeza zaidi.  Inakadiriwa kwamba binadamu wa kwanza wenye macho ya bluu waliibuka kati ya miaka  6,000 na 10,000 iliyopita.
Macho yenye rangi mbili
Hii husababishwa na ukosefu wa rangi (melanin) katika jicho moja kulifanya lilingane na jingine.  Kadiri ya watu sita miongoni mwa 1,000 huzaliwa na kasoro hiyo.  Mwigizaji wa kike wa Marekani, Mila Kunis, na mwimbaji Mwingereza, hayati David Bowie, ni mifano ya kasoro hiyo.

 

Comments are closed.