The House of Favourite Newspapers

YAJUE MAHABA YA WANAWAKE WA SIKU HIZI

Waliosema mapenzi yana-run  dunia hawakukosea kwa sababu kila mwaume anahitaji mwanamke wa kuwa naye katika safari ya maisha na kuwa naye kimapenzi lakini kwa baadhi ya wanawake wa wakati huu mambo yamekuwa ni changamoto ya hali ya juu.

 

Kwa mwanaume ambaye amekuwa kwenye mahusiano hivi karibuni lazima atakuwa ameshayaona au yameshamtokea mambo haya. Lakini kwa mwanamke atakayesoma hapa na anahitaji mapenzi ya kweli ni lazima ajirekebishe.

 

Utafiti mdogo umefanywa na kugundua baadhi ya wanawake wengi siku hizi hawaonyeshi mahaba yaani kwa ujumla hawako “romantic”. Wanawake wengi siku hizi akipata mwanaume anaona amepata mtu wa kumsaidia shida zake kwa hiyo hata akiwa ndani ya mahusiano anafikiria zaidi kutatuliwa shida zake kuliko mahusiano yenyewe.

 

Wanawake wa siku hizi wengi, kwa mfano umemtoa out kidogo mkapate walau msosi sehemu nzuri, mkianza kula mpaka mnamaliza hakumbuki hata kukulisha kidogo kimahaba. Unakuta anakula msosi kimpango wake utafikiri anakula na kaka yake. Mnatoka kidogo mnatembea unakuta anatembea na wewe utafikiri anatembea na kaka yake; yaani unaweza ukamuacha nyuma kidogo au akawa mbele yako anashindwa kujiongeza kupitisha mkono wake kwenye kikwapa chako na kukushika kimahaba.

 

Wakati mwingine anakuona jasho linakutoka usoni anashindwa hata kukufuta kimahaba anakutazama tu utafikiri wewe ni kinyago cha mpapure. Wakati anakuaga anaondoka utafikiri anamuaga kaka yake hakupigi hata busu. Mwanamke unazungumza naye hakushiki hata ndevu zako kimahaba, mwanamke unakuwa naye hakufanyii massage wala hakukati mara mojamoja kucha zako kimahaba.

 

Wakati mwingine unakuta umekaa naye mwaka mzima kwenye mahusiano lakini hajawahi kukwambia neno “Nakupenda” mpaka wewe uanze kumwambia kwanza.

 

Wanawake wengi wa siku hizi wanapenda kudekezwa, kubembelezwa na kupewa pesa, ndiyo maana wengi utasikia wakisema “nataka mwanaume romantic na mwenye pesa” lakini hawajiulizi je, wao ni romantic? Au sisi wanaume hatuhitaji hayo mahaba ya wanawake?

 

Asili ya mwanamke ni mfariji mkuu wa mwanaume lakini siku hizi wanawake wengi wamekuwa stress kwa wanaume.

 

Note: Hakuna mwanaume mbahili kwa mwanamke romantic.

 

Comments are closed.