The House of Favourite Newspapers

Yanga amueni kwa watu makini katika uchaguzi

 

KLABU ya Yanga inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu wake wa viongozi keshokutwa Jumapili. Huu ni wakati wa Yanga kufanya maamuzi sahihi katika wakati huu sahihi.

 

Natumia neon ‘sahihi’ kwa vile Wanayanga wanajua kipindi kigumu wanachopitia sasa cha klabu kutokuwa na fedha tangu aliyekuwa mwenyekiti wao, Yusuf Manji kujiuzulu.

 

Yanga imekuwa kama mwana asiyekuwa na mzazi kwani kuondoka kwa Manji kukafuatia na wimbi la viongozi kujiuzulu kulikosababisha sasa Yanga kuingia katika uchaguzi mkuu keshokutwa, uchaguzi ambao ni muhimu sana kwao.

 

Baada ya hapo Yanga imekuwa ikitembeza bakuli ili kuchangia klabu hiyo ili iweze kujiendesha kusafiri huku na huko na kulipa mishahara pia ya wachezaji wake ambao wamekuwa kama watoto yatima.

 

Wakati Yanga inaingia katika uchaguzi keshokutwa Wanayanga wanapaswa kukumbuka haya na kuona kuwa inapata watu sahihi wa kutengeneza mipango ya kuiondoa Yanga katika kutembeza kapu kwenda kuwa klabu inayojiendesha kisasa ambayo inajiendesha kisasa na kusubiri mafanikio makubwa mbeleni.

 

Na hii itatokana na Wanayanga wenyewe kufanya maamuzi sahihi keshokutwa. Yanga inahitaji watu wa kuleta mapinduzi makubwa kuifanya kuwa klabu inayojiendeshe kibiashara na siyo hivi kimaskini kwa kutembeza bakuli. Naamini huu ndiyo wakati mzuri kwa Wanayanga kufanya maamuzi sahihi keshokutwa ya kuchagua kiongozi sahihi ambaye anaweza kuwafikisha kule ambapo wanataka.

Timu hii inahitaji kiongozi ambaye atahakikisha kabla hajaondoka kwenye uongozi wake anaacha alama ya kukumbukwa, inahitaji kiongozi anayefahamu changamoto muhimu za timu hii. Yanga inahitaji kiongozi anayefahamu kuwa timu hiyo haina uwanja wa mazoezi na inakodi uwanja wa mechi, lakini inahitaji kiongozi ambaye ataweka umoja kwa viongozi wengine.

 

Jambo pekee ambalo kiongozi wa Yanga anatakiwa kufanya ni kuhakikisha timu hiyo inakuwa na mafanikio kimataifa, kufika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kufika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ni alama ambayo haiwezi kusahaulika kwenye timu hiyo kuliko ubingwa.

 

Yanga ina matatizo mengi kwa sasa na jambo lingine ni kwamba inafanya uchaguzi ikiwa inaelekea kwenye usajili kitu ambacho mashabiki wengi wanasubiri ni kuona inapata kiongozi gani ambaye anaweza kuwa na ushawishi wa wachezaji wapya, ili kuweza kupambana na timu nyingine kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa.

 

Simba wameonekana kuwa na kasi ya juu kwa kuwa wamekuwa na ushawishi mkubwa wa fedha, jambo ambalo Yanga nao wanatakiwa kufanya. Ni lazima uongozi unaingia Yanga ufahamu kuwa sasa aina ya soka limebadilika na fedha ndiyo kila kitu tofauti na hali ilivyokuwa hapo nyuma.

 

Sasa hivi hata ukihitaji mchezaji mzuri ni lazima ahakikishe kuwa timu ina uwezo wa kifedha, hivyo ni lazima uongozi utakaoingia uwe na ushawishi mkubwa kwa wadaui.

Comments are closed.