The House of Favourite Newspapers

Yanga, Azam Ubabe Ubabe Leo

Mshambuliaji wa timu ya Azam, Donald Ngoma (kulia) akiwa na Tafadzwa Kutinyu 

YANGA na Azam FC leo zitashuka kwenye Dimba la Amaan visiwani hapa huku kila mmoja akitamba kumchapa mwenzake kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani hapa.

 

Azam na Yanga zimepangwa kundi moja ambalo ni B katika michuano hiyo, na katika mechi zao za awali, Azam FC ilibanwambavu na Jamhuri ya Pemba ambapo walitoka sare ya bao 1-1 na Yanga ambao wamepeleka kikosi cha vijana, waliichapa KVZ bao 1-0.

 

Mara ya mwisho timu hizo kukutana kwenye michuano hiyo ilikuwa mwaka 2017, ambapo Azam iliichapa Yanga mabao 4-0. Wakati Yanga ikipeleka kikosi cha pili, Azam wenyewe wamepeleka ‘mziki’ kamili lengo likiwa ni kuhakikisha wanautwaa ubingwa huo ambapo wao ni mabingwa watetezi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha wa Azam FC, Hans van Der Pluijm, alisema: “Nimejiandaa vyema na mechi hiyo, kikosi changu kipo vizuri, nimetoa sare mchezo wa kwanza, hivyo nahitaji kushinda katika mchezo unaofuata, wachezaji wote wapo vizuri, nayafanyia kazi makosa ya mechi iliyopita ili kuweza kushinda.

 

” Naye Mratibu wa Yanga, Hafidhi Salehe, alisema: “Lengo la kocha Mwandila ‘Noel’ ni kuona timu inafanikiwa kupata ubingwa wa michuano hii, watu walidharau kikosi chetu lakini tumeweza kushinda na kupata matokeo ya bao moja, hivyo tunajipanga kushinda katika kila mechi ili turudi Dar na kombe.”

Comments are closed.