The House of Favourite Newspapers

YANGA HAIKAMATIKI, FEI TOTO APELEKA KILIO KMC, TAZAMA BAO LAKE – VIDEO

MABINGWA wa kihistoria Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa Saba kwa kuwafunga bao 1-0 KMC, mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

 

Mchezo huo ulikuwa na ushindani kwa timu zote ambapo iliwachukua dakika 89, Yanga kupata bao ambalo lilifungwa na kiungo mkabaji Feisal Abdallah “Fei Toto” baada ya kupiga faulo ya moja kwa moja iliyomshinda Juma Kaseja.

 

Ushindi huo unawarejesha Yanga kwenye nafasi ya pili kwa kuishusha timu ya Simba ambayo ina pointi 20 huku Yanga wakiwa na pointi 22, Azam ni vinara wakiwa wamekusanya pointi 24.

 

KMC wamecheza michezo 11 na wameshinda mchezo mmoja huku saba wametoa sare na wamepoteza michezo mitatu, Yanga wamecheza michezo nane, wameshinda michezo Saba huku wakitoa sare mchezo mmoja.

 

Mabadiliko kwa KMC: Dakika ya 73 ameingia Ramadhani Kiparamoto kuchukua nafasi ya Omary Ramadhani. Dakika ya anaingia James Msuva kuchukua nafasi ya Masoud Abdalla.

Mabadiliko kwa Yanga: Dakika ya 74 anatoka Thaban Kamusoko anaingia Amissi Tambwe.

GOLI la FEI TOTO KMC VS YANGA 0-1

Comments are closed.