The House of Favourite Newspapers

Yanga Mpya Wapiga Dili Kazi Wanayo

SIKU chache baada ya uongozi mpya wa Klabu ya Yanga kuingia madarakani na kuanza mikakati ya kukisuka upya kikosi cha timu hiyo, uongozi huo umekuja na mkakati kabambe kwa ‘wapiga dili’ wote waliokuwa wakitumia kipindi cha usajili kwa ajili ya kujinufaisha.

 

Mwenyeki wa klabu hiyo, Dkt. Mshindo Msolla amesema kuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanakabiliana na wote walikuwa wakitumia kipindi cha usajili kujinufaisha wenyewe hawapati tena nafasi hiyo.

 

Alisema kila kitu kinachohusiana na usajili kitafanywa na kocha kwa kushirikina na kamati husika ambayo itakuwa ikisimamia zoezi hilo bila ya kuwepo kwa mtu wa kati kama ilivyokuwa huko nyuma.

 

“Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kukisuka upya kikosi chetu na kila kitu kinachohusiana na usajili kitakuwa kikisimamiwa na kocha, hatutaki tena mambo ya mtu wa kati.

 

“Tunataka kuwa na kikosi bora kwa ajili ya kuiletea timu yetu mataji, kwa hiyo kocha ndiye atakayehusika zaidi katika zoezi zima la usajili akishirikiana na kamati ya usajili tutakayo iunda,” alisema Msolla.

Tambwe Afunguka kurogwa na Donald Ngoma

Comments are closed.