The House of Favourite Newspapers

Aubameyang Afananishwa na Henry

BEKI wa zamani wa Arsenal, Martin Keown amemfananisha Pierre-Emerick Aubameyang na nyota wa zamani wa kifaransa, Thierry Henry.

 

Aubameyang alipiga `hattrick’ wakati Arsenal ilipoiliza Valencia mabao 4-2 ugenini na kutinga fainali ya Ligi ya Europa, juzi. Ushindi huo uliifanya Arsenal kusonga mbele kwa jumla ya mabao 7-3 na sasa itacheza fainali dhidi ya Chelsea.

 

Keown, ambaye enzi zake alikuwa anasifika kama beki asiyekuwa na masihara Aubameyang ni mkali kama staa wa zamani wa Arsenal. Henry.

 

Henry ndio anashikilia rekodi ya kuifungia Arsenal mabao mengi zaidi, ambapo wakati akichezea timu hiyo, ambapo
alitupia mabao 228.

 

Keown alisema kuwa Aubameyang akiendeleza makali yake ya sasa basi atavunja rekodi ya Henry. “Mara nyingi ninasema kuwa Aubameyang anafanana uchezaji wa Henry na amedhihirisha tena hilo kwenye mechi hii na Valencia,” aliongeza Keown. Aubameyang tangu amejiunga na Arsenal ameifungia mabao 39 katika mechi 63.

Tambwe Afunguka kurogwa na Donald Ngoma

Comments are closed.