The House of Favourite Newspapers

Yanga SC Kuwafuata Waarabu Kesho

KIKOSI cha Yanga, kesho Alhamisi kinatarajiwa kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya wenyeji wao, USM Alger, huku Mghana akiwa mwamuzi wa kati.

Yanga ambayo kwenye michuano hiyo imepangwa Kundi D, mechi yake ya kwanza ni dhidi ya USM Alger itakayo­chezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Stade 5 Juillet 1962 uliopo kwenye Mji wa Algiers, Algeria.

 

Katika mchezo huo unaoanza ma­jira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Mghana, Daniel Nii Ayi Laryea ndiye atakuwa mwamuzi wa kati, aki­saidiwa na Mnigeria, Abel Baba, pamoja na David Laryea ambaye naye ni raia wa Ghana.

Akizungumzia safari yao hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alisema: “Timu itaondoka Alhamisi hapa Dar es Salaam kupitia Dubai na kwenda moja kwa moja Algeria tayari kwa huo mchezo.

 

“Tulifahamu kwamba tuna mchezo huo kwa sababu ratiba ya Caf ililetwa mapema, hivyo maandalizi ya sisi kwen­da kupata matokeo mazuri yalishaanza na tuna imani kwamba tutaanza vizuri hatua hiyo.”

Katika kundi hilo, mbali na USM Alger, pia Yanga imepangwa na Rayon Sports ya Rwanda na Gor Mahia kutoka Kenya.

Omary Mdose na Martha Mboma

Comments are closed.