The House of Favourite Newspapers

VEE MONEY Achekelea Views YouTube

Vanessa Mdee ‘Vee Money’,

MWANADADA ambaye kwa sasa anafanya vyema na album iitwayo Money Mondays, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, hivi karibuni amechekelea views katika mtandao wa YouTube ambazo wimbo wake namba 9, kwenye album yake uitwao Wet, umepata.

Wimbo huo ambao video yake ilifanywa na prodyuza kutoka Afrika Kusini, Justin Compas, ukiwa na wiki mbili tu umeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja jambo ambalo lilimfanya Vee Money kuandika hivi kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram;

“1 Million views in 2 weeks. #Wet. Kwangu mimi ni kitu kikubwa tena sana. (Nimesema kwangu mimi).”

Mbali na maandishi hayo Vee Money aliwashukuru pia mashabiki wake ambao wanampa sapoti katika kazi zake za muziki kila kukicha.

TORI: BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.