The House of Favourite Newspapers

Yanga Simba Hakuna Mbabe, Watoka Sare

0

Mechi ya Kariakoo Derby ambayo ni ya Ligi Kuu Bara,  kati ya Watani wa Jadi Yanga Sc dhidi ya Simba Sc imemalizika leo jioni Novemba  7, kwenye dimba la Mkapa kwa sare ya bao 1-1, mechi ambayo imewafanya mashabiki kupokezana kushangilia, wana Jangwani wakicheza kipindi cha kwanza na Mnyama kipindi cha pili.

Yanga walianza vizuri kipindi cha kwanza   na Kocha Kaze alifanikiwa na mpango mkakati wa kuwasubiri Simba  na kutumia mashambulizi ya kushtukiza kwa kasi, mashambulizi ambayo yaliwapa wakati mgumu mabeki wa kati wa Simba Paschal Wawa na Joash Onyango.

Mashambulizi hayo yalifanikiwa kupata bao kwa mkwaju wa penati iliwekwa wavuni na mshambuliaji Michael Sarpong, baada ya mlinzi wa kimataifa wa Kenya  Onyango kucheza faulo ambayo mwamuzi wa kati aliamuru kuwa penati.

 

 

Kipndi cha pili Simba walionekana kubadilika na kuanza kushambulia kwa kasi tofauti na kipindi cha kwanza ambapo walionekana kutengeneza mashambulizi yao kwa taratibu na kuingia kwa Hassan Dilunga kuliifanya Simba kucheza kwa kasi.

 

Wakati mashabiki wengi wakiamini kuwa mechi inaisha kwa sare, Simba walisawazisha kupitia kwa Joash Onyango kwa kichwa akiunganisha mkwaju wa kona ya Luis Miquissone na kufanya matokeo kuwa 1-1.

 

Kwa matokeo ya leo Yanga amefikisha pointi 24 nyuma kwa pointi moja kwa vinara Azam fc wenye pointi 25, wekundu wa msimbazi wanaendelea kushika nafasi ya tatu kwa alama 20.

 

Leave A Reply