The House of Favourite Newspapers

Yanga Waingia Mzigoni, Wapania Kuiangamiza Mbao FC

Yanga wakijifua.

KIKOSI cha Yanga chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Mzambia, George Lwandamina leo kimeendelea kujifua kwenye mazoezi ya uwanjani.

Mazoezi yakiendelea.

Hiyo, ikiwa ni siku moja watoke kwenye mazoezi ya gym waliyofanya kwa muda wa siku mbili mfululizo Jumatatu na Jumanne. Timu hiyo, inajifua kwa ajili ya kujiandaa na mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

 

Kazikazi vijana wa Jangwani.

Katika mazoezi hayo ya leo asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Lwandamina alionekana akiwapa mbinu mbalimbali wachezaji wake ya jinsi ya kushambulia na kulinda goli lao.

Makipa wakijifua.

Kwenye mazoezi hayo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko alikuwepo nje uwanja akifuatilia mazoezi hayo ambaye yupo nje kwa muda wa wiki mbili akiuguza majeraha ya goti. Timu hiyo, kesho Alhamisi asubuhi inaendelea na mazoezi ya pamoja kwenye uwanja huo wa Uhuru .

Comments are closed.