The House of Favourite Newspapers

Yanga Waipa Kichapo cha Bao 2-1 Ruvu Shooting (Pichaz+Video)

yanga-na-ruvu-shooting-1 yanga-na-ruvu-shooting-2 yanga-na-ruvu-shooting-3 yanga-na-ruvu-shooting-4 yanga-na-ruvu-shooting-5 yanga-na-ruvu-shooting-6 yanga-na-ruvu-shooting-7 yanga-na-ruvu-shooting-8 yanga-na-ruvu-shooting-9 yanga-na-ruvu-shooting-10 yanga-na-ruvu-shooting-11

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga leo imeichapa timu ya maafande wa Ruvu Shooting kwa bao 2-1, mchezo wa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Vodacom ambao umepigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi na wa kusisimua, Ruvu Shooting ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kunako Dakika ya 8 kupitia kwa Mussa, alipata mpira kutoka upande wa kushoto kwa Yanga na kupiga shuti kali ambalo lilimshinda kipa wa Yanga.

Baadaye kunako Dakika ya 32, Simon Msuva akaisawazishia klabu yake ya Yanga, akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Haruna Niyonzima aliyetoa pasi murua na Msuva akikwamisha mpira wavuni baada ya mabeki wa Ruvu kujichanganya.

Mpaka timu zinakwenda mapumziko matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1. Wakati timu zinarejea uwanjani kipindi cha pili, Kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm alitolewa kwenye benchi la ufundi na mwamuzi kwa kile kinachodhaniwa kuwa alitoa maneno yasiyo mazuri kwa mwamuzi huyo, benchi la Yanga likasimamiwa na Kocha Msaidizi, Mwambusi.

Mpira uliendelea kuchezwa ambapo Dakika ya 52, Yanga wakapata bao la pili la kupigilia msumari wa ushindi, mfungaji akiwa ni Haruna Niyonzima baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Donald Ngoma ambaye aliyempa pasi kisha Niyonzima akapiga shuti kali lililojaa wavuni. Mpaka dakika 90 zinakwisha Yanga 2-1 Ruvu Shooting.

Kwa matokeo ya leo Yanga wanabaki nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 33, pointi mbili nyuma ya vinara wa ligi hiyo Wekundu wa Msimbazi Simba SC.

PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

whatsapp-image-2016-11-14-at-10-00-10

Comments are closed.