The House of Favourite Newspapers

Yanga Wapokea Rasimu ya Mabadiliko

0

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Yanga leo Desemba 2, 2020,  imepokea ripoti kwa ajili ya mabadiliko ya uendeshwaji wa kisasa baada ya ushauri wa La Liga.

 

Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM ambao pia ni wadhamini wa Yanga, Injinia Hersi Said, alisafiri kuelekea nchini Hispania kwa ajili ya kuchukua ripoti hiyo kabla ya kuikabidhi kwa mwenyekiti  leo.

Ripoti hiyo yenye kurasa 400 itaenda kuchakatwa katika Kamati ya Utendaji  na Kamati ya Sheria na Kamati ya Mabadiliko kabla  ya kupelekwa kwa wanachama kupitia matawi nchi nzima ili utaratibu uwe shirikishi.

 

Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Mshindo Msolla, amesema mchakato huo utafuata sheria na taratibu zote za nchi kama ulivyoelezwa na baadaye wataitisha mkutano mkuu wa mwaka ili kupitisha mabadiliko hayo.

 

Amesema ripoti hiyo amemkabidhi Senzo Mbatha ambaye ni mshauri wa klabu na ndiye ataongoza kuelekea mabadiliko hayo ingawa bado itabaki kuwa mali ya wanachama.

Leave A Reply