The House of Favourite Newspapers

Mwinyi Ateua Wakuu wa Mikoa

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Mwinyi,  jana Desemba Mosi, 2020,  ameteua wakuu wa mikoa, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 61 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, na uteuzi huo umeanza leo Jumanne, Desemba Mosi 2020.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, walioteuliwa ni Idrissa Kitwana Mustafa, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi; Ayoub Mohammed Mahmoud (Kaskazini Unguja) na Rashid Hadid Rashid (Kusini Unguja).

 

Wengine ni Salama Mbarouk Khatib (Kaskazini Pemba) na  Mattar Zahor Masoud (Kusini Pemba).

Leave A Reply