The House of Favourite Newspapers

Yanga Wataka Mtaro Unaoharibu Uwanja wa Kaunda Ukarabatiwe

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo.

Kifusi kinachojazwa katika uwanja wa Kaunda kwa ajili ya ujenzi ili uanze kutumika kwa mazoezi.
Taswira ya jumla ya uwanja huo.
Baadhi ya eneo ambalo limekwisha wekwa kifusi katika uwanja huo.

 

UONGOZI wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, umeiomba Manispaa ya Ilala kuufanyia ukarabai mtaro unaotiririsha maji taka yanayoelekezwa kwenye uwanja wa klabu hiyo wa soka wa Kaunda ambao kwa sasa umejaa magugumaji.

Uwanja huo kwa sasa unafanyiwa ujenzi kwa kujaza kifusi cha udongo ili uweze kuanza kutumika katika mazoezi ya timu hiyo.

Akizungumza leo Jumamosi jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga ambaye ni msimamizi wa ujenzi huo, Charles Mkwasa, amesema licha ya mchakato huo kuendelea vizuri, wamekuwa wakikerwa na mtaro huo ambao wameshaulalamikia mara kibao kwa mamlaka husika bila ya mafanikio yoyote.

“Mtaro huo unatoa majitaka na maji ambayo yanavuja katika eneo hilo kwa kuwa hayaendi kwenye mtiririko unaonatakiwa na matokeo yake yanajaa kwenye eneo la uwanja na kusababisha ukuta ambao ulikuwa unazuia, uanguke hivyo sasa yanajaa ndani,” alisema Mkwasa.

Comments are closed.