The House of Favourite Newspapers

Yanga ya Zahera inavunja Rekodi Tu

YANGA imefanikiwa kuvunja rekodi yake ya msimu uliopita ya kumaliza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 52 lakini msimu huu katika mechi 19 imeshavuna alama 53.

Timu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya Mkongoman Mwinyi Zahera, imekuwa ya tofauti ukilinganisha na msimu uliopita ambapo kitakwimu haikuwa vizuri na ilimaliza ilishika nafasiya tatu mwishoni mwa msimu nyuma ya Simba na Azam FC.

Ni wazi msimu huu Yanga huenda ikazidi kutengeneza rekodi mpya baada ya sasa kufanikiwa kuvunja rekodi yao ya msimu uliopita.

 

Yanga msimu uliopita ilimaliza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 52 katika michezo yake 30 ambayo ilicheza lakini kasi ya safari hii inaonekana kuwa kubwa licha ya kuwa wamekuwa hawachezi soka la kumiliki mpira muda mwingi. Msimu uliopita walishinda mechi 14, wakipoteza michezo sita na wakifunga mabao 44.

 

Msimu huu mambo yamekuwa tofauti kwao licha ya pointi 53 katika mechi 19 wamefunga mabao 38. Msimu huu Yanga itacheza mechi 38 badala ya 30 kama ilivyokuwa awali lakini sasa imeshinda mechi 17 na sare mbili bila kupoteza mechi yoyote.

 

Yanga ndiyo wanaongoza katika msimamo wa ligi kuu wakiongoza kwa tofauti ya pointi 12 dhidi ya Azam FC ambayo inashika nafasi ya pili.

Comments are closed.