The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaendeleza Ubabe Ligi Kuu ya NBC, Yaichapa Dodoma Jiji

0
Nyota wa Yanga Fiston Mayele akipambania mpira katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji

Klabu ya Yanga imeendeleza ubabe wake kwenye Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya klabu ya Dodoma Jiji, pambano ambalo limechezwa kwenye Uwanja wa CCM Liti mkoani Singida.

 

Mabao ya yote mawili ya Yanga yamewekwa kimiani na mshambuliaji Fiston Mayele ambaye kwa sasa ndiye kinara wa mabao akiwa na jumla ya mabao 8.

 

Kwa matokeo hayo Yanga inarejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na jumla ya alama 29 sawa na Klabu ya Azam lakini Yanga inaongoza kwa tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa huku pia ikiwa imecheza michezo 11 wakati huo Azam wakiwa tayari wameshacheza michezo 13.

Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika Uwanja wa CCM Liti mkoani Singida

Nafasi ya tatu inashikiliwa na Klabu ya Simba ambayo ina jumla ya alama 27 ikiwa tayari imeshacheza michezo 12 huku kesho ikitarajiwa kuvaana na Mbeya City katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.

 

Aidha Yanga imefanikiwa kufikisha jumla ya michezo 48 ya Ligi Kuu ya NBC bila kupoteza mchezo (Unbeaten).

Leave A Reply