The House of Favourite Newspapers

Yanga Yafanyia Kazi Mapungufu Yake, Sasa ni Kipigo Kila Nayekuja – Video

0

KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi, Jumamosi iliyopita aliiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kukabidhiwa mikoba, akaambulia sare ya 1-1 dhidi ya KMC.

 

 

Sasa baada ya mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Mwambusi amesema atafanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United utakaochezwa kesho, uwanjani hapo.

 

“Tumeshafanyia Kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo uliyopita na tupo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Biashara United, mkakati wetu katika mechi kumi (10) zilizobakia ni kuvuna alama tatu (3) kwenye kila mchezo,” amesema Mwambusi.

 

Mwambusi ambaye anaiongoza Yanga baada ya Kocha Cedric Kaze kutimuliwa Machi 7, mwaka huu, amezitaja sehemu ambazo zimeonekana kuwa na matatizo sugu kwamba ni safu ya ulinzi na ushambuliaji.

 

Leave A Reply