The House of Favourite Newspapers

Yanga Yatinga Fainali Mapinduzi, Yaichapa Azam

0

TIMU ya Yanga imefanikiwa kutinga kwenye Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2021, baada ya kuichapa Azam FC kwa mikwaju ya penati 5-4 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Aman Zanzibar, ambapo ndani ya dakika tisini timu hizo zilifungana bao 1-1.

 

Vijana wa Kocha Cedric Kaze walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 51 kupitia kwa Tuisila Kisinda ‘TK Master’.

 

Wana lambalamba walifanikiwa kuchomoa goli hilo kupitia kwa Obrey Chwira akitumia vema uzembe wa mlinda mlango wa Yanga, Farouk Shikalo.

 

 

Kwenye mikwaju ya penati timu ya ‘Wananchi’ walifanikiwa kuibuka na ushindi baada ya kupata penati 5-4 huku Shikalo akiibuka shujaa baada ya kuokoa mikwaju miwili.

 

Yanga inasubiri mshindi kati ya ‘mnyama’ Simba ambaye anaingia dimbani saa 2:30 usiku kukipiga dhidi ya Namungo FC.

Fainali ya Kombe la Mapinduzi itachezwa  Januari 13 kwenye Uwanja Aman Zanzibar.

Leave A Reply