The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaingia Mkataba wa miaka miwili na Shirika la Ndege la ATCL – Video

0

Klabu ya Yanga imengia Mkataba wa miaka miwili na Shirika la Ndege la ATCL, wenye makubaliano ya kubadilishana huduma ambapo Yanga itapata punguzo la gharama za Usafiri na kuitangaza ATCL kwenye Safari zao.

Mbali na kuitangaza ATCL, pia Yanga wataitangaza Tanzania ikiwa ndio lengo Mama la Mkataba huo, amezungumza Mtendaji Mkuu wa ATCL Ladislaus Matindi.

“Tumesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitangaza Air Tanzania katika kipindi chote hicho. Nasi kama Young Africans SC tuna matumaini makubwa kuwa tutaendelea kunufaika na huduma bora za shirika hili kwa bei punguzo. Tunatambua mchango mkubwa wa Air Tanzaniakwa Klabu yetu nasi tunao wajibu wa kuwaunga mkono”- Rais Eng.Hersi Said

“Tumekuwa na ushirika na Young Africans SC kwa muda mrefu sana, lakini kwa sasa tumeona umuhimu wa kuyaweka katika mfumo rasmi. Mkataba huu msingi wake haswa ni mabadilishano ya huduma. Ushirika huu faida yake sio tu kwa @airtanzania_atcl bali hata kwa vivutio vyetu vya utalii ambavyo tumekuwa tukivitangaza” Mhandisi Ladislaus Matindi – CEO Air Tanzania

Leave A Reply