The House of Favourite Newspapers

Yanga Yamfuatilia Kipre Tchetche

0

 

Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC anayechezea Al Nahdha ya Oman, Kipre Tchetche.

YANGA imeamua kufunga safari na kwenda nchini Ivory Coast kumfuatilia mshambuliaji wa zamani wa Azam FC anayechezea Al Nahdha ya Oman, Kipre Tchetche ili iweze kumsajili. Hatua hiyo ya Yanga imekuja siku moja tu tangu watani zao Simba

kuanza mazungumzo na beki wa zamani wa Azam FC, Pascal Wawa ambaye pia ni raia wa Ivory Coast. Yanga hivi sasa ipo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chake kinachojiandaa na Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika. Mmoja wa mabosi wa Yanga, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, wanataka kumsajili Tchetche kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya

ushambuliaji baada ya winga wao, Simon Msuva kupata ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. Mtoa taarifa huyo alisema, tayari kigogo mmoja anayeshughulikia mambo ya usajili amesafiri kwenda Ivory Coast kumalizana na Tchetche mwenye sifa ya kuwa na kasi na nguvu za kupiga mashuti ya mbali. “Msuva wakati wowote anaondoka na tumekubali kumwachia aende Morocco, hivyo ni lazima tumpate

mchezaji wa kuziba nafasi yake. “Tutampata mchezaji huyo (Tchetche) kutokana na fedha za mauzo ya Msuva na katika kuhakikisha tunampata mchezaji wa aina yake, uongozi umempendekeza Tchetche ambaye anaweza kutokea pembeni kama kiungo mshambuliaji,” alisema bosi

huyo. Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa kuzungumzia usajili huo, kama kawaida alisema: “Hayo masuala ya usajili anayehusika ni Nyika, yeye anaweza akazungumzia vizuri.” Yanga kama itafanikisha usajili wa Tchetche itakuwa na washambuliaji wanne wa kigeni ambao ni Donald Ngoma (Zimbabwe), Obrey Chirwa (Zambia), Amissi Tambwe (Burundi) na Tchetche wa Ivory Coast.

Wilbert Molandi | Championi Jumamosi

Leave A Reply