The House of Favourite Newspapers

Yanga Yampa Hofu Mkude

BAADA ya kutoa sare dhidi ya Mwadui FC, kiungo wa Simba, Jonas Mkude, ameingiwa na hofu ya kushushwa kileleni na Yanga kutokana na kasi ambayo wamekuwa nayo kwa michezo yao ya hivi karibuni kwa kupishana alama tano.

 

Simba kwa sasa ina pointi 42 huku Yanga wao wakiwa na alama 37 na wote wakiwa wamecheza michezo 18 kila mmoja mpaka sasa kwenye ligi hiyo.

Kiungo huyo, Mfaransa amekubali uwezo wake hasa katikati na kutaja kuwa kwake ndiyo kiungo bora kwa sasa mwenye uwezo mzuri.

 

Mkude alisema kuwa ni lazima wapambane kwa bidii, bila hivyo basi wapinzani wao wa­naweza kuwaondoa kwenye ile nafasi kutokana na kasi ambayo wamekuwa wakiionyesha kwa sasa.

 

Yanga wameshinda mechi tano mfululizo tangu walivy­oanza kwa kuichapa Ruvu Shooting mabao 0-1 jijini Dar es Salaam Januari 21, mwaka huu.

 

“Ni lazima tufanye vi­zuri kwani tukicheza Yanga ambao wapo nyuma yetu na sasa wanafanya vizuri wanaweza kutushu­sha kwa hiyo ni lazima tuhakikishe tunashinda kila mch­ezo uliopo mbele yetu.

 

“Hakuna timu ya kudharau iwe nyum­bani au ugenini, cha msingi ni kujipanga ili kuweza kuwa imara na kujikita zaidi pale juu kwa alama nyingi zaidi na pia Azam siyo wa kuwad­harau, wanaweza kufanya lolote,” alisema Mkude.

Martha Mboma, Dar es Salaam

Comments are closed.