The House of Favourite Newspapers

Yanga Yamtoa Chirwa Kwa Mkopo, Yasajili Mbadala

img_20160630_091233Mshambuliaji wa Yanga raia wa Zambia Obrey Chirwa.

Klabu ya Yanga imemtoa kwa mkopo mshambuliaji wake raia wa Zambia Obrey Chirwa kwenda katika klabu ya Platinum ya Zimbabwe.

Taarifa kutoka ndani ya klabu Yanga imesema kuwa makubaliano hayo yalifikiwa dakika chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa usiku wa saa 5:59 siku ya jana (Desemba 15, 2016)

Taarifa hizo zimebainisha kuwa klabu hiyo imemsajili straika kutoka katika klabu ya Zesco, anayefahamika kwa jina
Winston Kalengo kama mbadala wa Chirwa.

Kwa mujibu wa makubaliano katika mkopo huo, Yanga itakuwa ikimlipa Chirwa nusu mshahara, na nusu nyingine itakuwa ikilipwa na Platinum.

Chirwa ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa kishindo katika klabu hiyo, ikidaiwa kuwa ndiye aliyekuwa mchezaji ghali zaidi akisajiliwa kwa dau la shilingi za kitanzania milioni 240, lakini hakuwa na mwanzo mzuri katika ligi kuu Tanzania Bara licha ya kuanza kufunga katika michezo ya mwisho ya mzunguko wa kwanza.

Hadi anaondoka klabuni hapo ameifungia mabao matano.

Aunt Ezekiel: Siku ya Kwanza Kufanya Mapenzi na Moze Iyobo, Tulikuwa Tunaangalia TV

Aunt Ezekiel: Kama Nina Mimba, Hairudi Ndani, Itatoka Nje

Comments are closed.