The House of Favourite Newspapers

Waziri Jafo: Takwimu Zinaonesha Watu Milioni 4 Afrika Wanapoteza Maisha Kwasababu Ya Nishati Chafu

0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo (katikati), Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ( wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia wa Oryx mmoja wa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dk.Selemeni Jafo amesema takwimu zinaonesha watu milioni nne barani Afrika wanapoteza maisha kwasababu ya kutumia nishati chafu ikiwemo ya kuni na mkaa.

Hivyo amesema ajenda ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kuanzisha kampeni ya kuhamasisha nishati safi Afrika inapaswa kuungwa mkono na watu wote huku akitumia nafasi hiyo kueleza matumizi ya kuni na mkaa nchini yanasababisha hekta 46242 kupotea kila mwaka kwasababu ya kuni na mkaa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali Dk.Jafo amesema hatua hiyo inakwenda kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kampeni ya kuhamasisha nishati safi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha.

“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amekuwa na dhamira njema na ndio maana amekuja na kampeni ya nishati safi ya kupikia.Haya ni mapenzi yake na kwasababu tunafahamu nishati chafu inamadhara makubwa katika mazingira.

“Kwanza watu wanalazimika kutegemea kuni na mkaa kwa hiyo kuna uharibifu wa mazingira.Takwimu zinaonesha kila mwaka hekta 46242 zinapotea kwasababu ya kuni na mkaa,”amesema Dk.Jafo.

Pia amesema takwimu zinaonesha kuwa kina mama na wasichana kwa asilimia kubwa wanatumia wastani wa saa 20 kwa wiki kwa ajili ya kutafuta kuni na mkaa au wakati mwingine ni kinyesi cha wanyama.

“Leo hii ukiona nchi imejipanga katika nishati safi ya kupia ni jambo la msingi lenye kutia matumani.Watafiti wanatuambia kitendo cha kutumia nishati safi ya kupikia kwa akina mama wajazito kunasaidia kurekebisha presha ya mama mjazito,”amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman akiwa na watumishi wa Kampuni ya gesi ya Oryx wakiwa kwenye picha ya pamoja na mama lishe na baba lishe wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha.

Ameongeza pia nishati safi inasaidia mama mjazito kupata mtoto mwenye uzito unaokubalika anapozaliwa , hivyo kuna faida nyingi kutumia nishati safi ya kupikia.

“Nina fahamu mpaka leo hii Oryx wameshatoa mitungi ya gesi 32,000 kwa ajili ya jamii na wameshatumia Sh.bilioni 2.7 lakini bado wameendelea kuendelea na kampeni hiyo kwa kutoa mitungi kwa jamii.

Ameongeza kuwa Oryx wamekuwa mfano mzuri kuifikia jamii huku akifafanua tayari Serikali imeshatoa maelekezo kwa taasisi zinazoanzia watu 100 kufunga mfumo wa kutumia nishati safi ya kupikia na tayari taasisia na mashirika ya umma yameanza kutumia nishati hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia kuhamasisha nishati safi ya kupikia wameona ni vema kuendelea kuyagusa makundi mbalimbali katika jimbo hilo.

Amesema kuwa kabla ya kugawa mitungi hiyo 1,500 ya Oryx kwa wana Arusha Mjini, tayari ameshagawa pia mitungi 1400 kwa wajasiriamali huku akisisitiza wataendelea na kuyafikia makundi yote yakiwemo ya watoto wanaolelewa vituo vya ya watoto yatima.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman amemetumia nafasi hiyo kuelezea madhara yanayotokana na kutumia kuni na mkaa ambapo amesema nchini Tanzania, wananchi 33,000 wanapoteza maisha kila mwaka kwa kuvuta moshi na chembe chembe zinazotokana na mkaa na kuni. Kupika na gesi ya Oryx itatatua jambo hili.

Aidha amesema kupika kwa kutumia gesi ya Oryx huzuia ukataji miti, kwa hiyo husaidia kulinda mazingira huku akieleza pia kutumia gesi ya Oryx huzuia wanawake kutumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa msituni.

“Kupika kwa kutumia gesi ya Oryx ni kupika kwa haraka na kwa ufanisi zaidi; kwa hiyo, wanawake wataanda chakula kwa wakati na wanaume hawatalalamika juu ya kuchelewa kwa chakula kinachosababisha mizogo.

kwa upande mwingine wajasiriamali Asha Mtumwa na Karim Abdallah wamesema ni jambo la kupongeza kuona Oryx inawakabidhi mitungi hiyo kwani inaenda kuondoa athari ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa matumizi ya kuni na mkaa ambapo inaathari kuanzia.

Leave A Reply