The House of Favourite Newspapers

Yanga Yamuacha Chirwa Dar

Kikosi cha timu ya yanga.

KIKOSI cha Yanga, jana kilielekea Kenya kwa ajili ya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup huku kocha msaidizi, Shadrack Nsajigwa, Obrey Chirwa na Kelvin Yondani wakibaki Dar.

 

Mbali na hao, pia Andrew Vincent ‘Dante’, Obrey Chirwa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Geofrey Mwashiuya, Juma Abdul, Emmanuel Martin, Gadiel Michael na Beno Kakolanya, wameachwa Dar.

Yanga imeenda Kenya kushiriki michuano hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa na yanatarajiwa kuanza keshokutwa Jumapili.

 

Wachezaji walioondoka ni makipa, Youthe Rostand na Ramadhan Kabwili, mabeki Ramadhan Kessy, Mwinyi Haji, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Pato Ngonyani na Said Juma Makapu.

Viungo ni Pius Buswita, Baruan Akilimali, Said Mussa, Raphael Daud, Papy Tshishimbi, Thaban Kamusoko na Maka Edward huku washambuliaji wakiwa ni Yusuph Mhilu, Matheo Anthony, Amissi Tambwe, Juma Mahadhi, Ibrahim Ajibu na Yohana Nkomola.

 

Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila, alisema: “Hatukuwa na muda mrefu wa kujiandaa, tulifanya maandalizi kwa siku moja kabla ya leo (jana) kuondoka.

“Ni kombe la wadhamini hivyo hatuwezi kuepuka kushiriki japo limekuja mwisho wa ligi ambapo wachezaji walihitaji kupumzika, kwa sasa tunatakiwa kuangalia nini cha kukifanya katika michuano hiyo na kama unavyojua inachezwa kwa staili ya mtoano, hivyo tutapambana.”

 

Kabla ya Yanga kuondoka jana jioni, asubuhi Simba nayo ilikwea pipa kuelekea Kenya kushiriki michuano hiyo.

Kikosi cha Simba kilichoondoka chini ya Kocha Mkuu, Mfaransa, Pierre Lechantre na Kocha Msaidizi, Mrundi, Masoud Djuma, ni makipa Aishi Manula, Said Mohamed ‘Nduda’ na Ally Salim. Mabeki Ally Shomary, Shomari Kapombe, Paul Bukaba, Erasto Nyoni, Yusufu Mlipili na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

 

Viungo ni Jonas Mkude, Rashid Juma, Said Ndemla, Haruna Niyonzima na Mohamed Ibrahim. Washambuliaji ni Marcel Boniventure Kaheza na Moses Kitandu.

John Bocco, Adam Salamba, Mzamiru Yassin na Shiza Kichuya ambaye mkataba wake umemalizika na kukiwa na taarifa za kutaka kuondoka kikosini hapo, wamebaki Dar.

Comments are closed.