The House of Favourite Newspapers

Yanga Yapewa Ufalme Mpya ligi kuu Baada ya Kupata Ushindi wa Mabao 5-0

0

 

Kikosi cha timu ya Yanga.

YANGA kwa sasa ni kama wamepewa ufalme wao kwenye ligi kuu baada ya kutabiriwa kufanya makubwa msimu huu, huku wakianza kwa kupata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya KMC.

Katika Ligi Kuu Bara ambapo Yanga ni mabingwa watetezi, Simba ni vinara wakiwa na pointi sita wakicheza mechi mbili, Yanga ina pointi tatu kunako nafasi ya nne baada ya kushuka dimbani mara moja.

Akizungumza na Spoti Xtra, beki wa zamani wa Simba na Yanga, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ amesema kulingana na jinsi ambavyo Yanga wameanza msimu kwa nguvu kubwa na ubora wa wachezaji waliouonesha, kama wataendelea kuwa hivyo anaamini watafanya vema na kuendeleza ufalme wa kutwaa ubingwa wa ligi.

“Yanga wamekuwa na mwanzo mzuri, kwa jinsi ambavyo wamecheza wameonesha kuwa kuna kitu wanakitaka kupitia ligi kuu msimu huu, wachezaji wamecheza vema na wameonesha kila mmoa kutamani kupata nafasi ya kucheza.

“Pengine labda mambo yaende tofauti, lakini kwa jinsi ambavyo wamecheza, naamini wataweza hata kuutetea ubingwa wao japo ni mapema sana,” alisema mkongwe huyo.

ALI KAMWE AMPIGIA SALUTI MAX – ”UKIKUTANA na SHABIKI wa KOLO USIBISHANE NAYE”…

Leave A Reply