The House of Favourite Newspapers

Yanga Yashusha Kiungo Msauzi

AKILI za viongozi wa Yanga zinaonekana hazipo tena kwenye Kombe la Shirikisho inayoendelea, kwani jana wachezaji waligoma lakini kuna kiungo kutoka Afrika Kusini aliyejulikana kwa jina la Kingsley ametua kusajiliwa.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo irejee nchini ikitokea Kenya ilipokwenda kucheza na Gor Mahia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Yanga walifungwa mabao 4-0. Jana wachezaji waligoma kufanya mazoezi wakishinikiza wapewe chao lakini viongozi wanaonekana kuangalia zaidi msimu ujao.

 

Yanga tayari imesajili wachezaji sita hadi hivi sasa ambao ni Mohamed Issa ‘Banka’, Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Jaffary Mohamed, Heritier Makambo na Fei Toto .

Kocha Mkuu wa timu hiyo Mkongoman, Mwinyi Zahera alisema kiungo huyo alitua hivi karibuni kwa siri nchini akitokea Sauzi alipokuwa akicheza soka kabla ya kukabidhiwa na kuanza majaribio.

 

“Bado viongozi wanaendelea na usajili wao na kama unafahamu tayari nimewashauri viongozi wasajili wachezaji wengine watatu wenye uzoefu wa michuano ya kimataifa na kitaifa kwa ajili ya kukiimarisha kikosi changu.

“Nimempokea mchezaji mwingine mpya kutoka Afrika Kusini ambaye nimekabidhiwa na kuanza naye mazoezi kabla ya kwenda Kenya. Kiukweli ni mchezaji mzuri aliyekuwa akicheza kwenye moja ya klabu ya Afrika Kusini inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo ambayo jina lake nimelisahau kidogo.”

MUSA MATEJA NA WILBERT MOLANDI

Comments are closed.