YANGA YASHUSHA MASHINE TATU MPYA

YANGA imempa ruhusa Kocha Mwinyi Zahera, kumalizana na mastaa watatu wa kigeni aliokuwa anawataka na wiki ijayo akisharudi Dar es Salaam  watamfuata nyuma kuja kumwaga wino. Spoti Xtra linajua Zahera ambaye sasa yuko kwenye timu ya taifa ya DR Congo akiwa kocha msaidizi amependekeza straika na kiungo Mkongo pamoja na winga Mghana ambao wote alishafanya nao mazungumzo ya awali akawa amekwama kutokana na fedha. Guylain Kisombe

Makuntima ndiye kiungo aliyekuwa akicheza Gabon na sasa karudi FC Lupopo ambaye Zahera anamtaka aje kuchukua namba ya Pappy Tshishimbi anayelalamikiwa na kocha huyo kwamba hafuati maelekezo na anacheza mpira wa shoo. Mbali na huyo pia winga anayemleta amekuwa akisisitiza

kwamba ni mwenye kasi na uwezo wa kupandisha mashambulizi na kutupia kwa maelezo kwamba Ibrahim Ajibu amekuwa akikosa mtu kama huyo. Katika maelezo yake ya kiufundi amekuwa akililia straika mtupiaji zaidi ya Heritier Makambo ambaye amekuwa akimuangusha katika mechi za hivi karibuni. Zahera ambaye familia yake inaishi Ufaransa, aliushukuru uongozi wa Yanga kwa kuafi kiana na mapendekezo yake na kumtaka afanye nao mawasiliano waje Dar haraka akishatua yeye. “Natarajia siku

chache baada ya kurudi Tanzania nitawapokea na mara moja kuanza nao maandalizi ya ligi na mambo mengine. “Yanga inapitia katika wakati mgumu sana jambo ambalo linawafanya hata wachezaji wangu

kujikuta wakipoteza morali, ila najua hili ni suala la muda tu siku si nyingi tutakuwa katika wakati mzuri hasa kama tutasajili wote hao niliowapendekeza kwenye dirisha hili dogo,” alisema Zahera. Yanga angalau imeanza kupumua baada ya Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kukubali kurejea Jangwani ingawa bado mamlaka za soka zimesisitiza hazimtambui

Toa comment