The House of Favourite Newspapers

Yanga Yatenga Bilioni 1 Kushusha Majembe

0

UKISIKIA jeuri ya fedha ndio hii sasa kwa Yanga kwani unaambiwa uongozi wa timu hiyo ukishirikiana na wadhamini wao, Kampuni ya GSM na SportPesa wamepanga kutumia kiasi cha shilingi bilioni moja na nusu kwa ajili ya usajili katika dirisha kubwa la usajili msimu ujao.

 

Yanga tayari wameridhia kumuachia kocha wao mkuu, Mbelgiji, Luc Eymael mikoba ya usajili kama ambavyo kocha huyo aliuomba uongozi kutokana na kufahamiana na wachezaji wengi wakubwa barani Afrika.

Kocha huyo ambaye hivi karibuni alilalamikia viwango vya wachezaji ndani ya timu hiyo, litakuwa jambo la kufurahisha kwake kupata kiasi hiko cha fedha kwani anataka kuboresha timu hiyo inayosuasua haswa katika eneo la ushambuliaji.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, alisema kupitia wadhamini wao GSM pamoja na SportPesa, wamekubali kuitengea timu hiyo kitita cha shilingi bilioni moja na nusu ambacho kitakuwa maalumu kwa ajili ya kusajili wachezaji msimu ujao.

 

“Kama ambavyo mnafahamu kuwa Yanga bado haijafikia ambapo Wanayanga tunapataka, hivyo kupitia wadhamini wetu ambao wanania ya kuifanya Yanga iwe ya moto, namaanisha GSM na SportPesa, kwa pamoja wameamua kututengea kitita cha shilingi bilioni moja na nusu kwa ajili ya kuboresha kikosi chetu kwenye usajili wa dirisha kubwa.

 

“Kiasi hiko kinaweza kuongezeka kutokana na mahitaji ya mwalimu na wachezaji ambao
atawahitaji, kutokana na wadhamini wetu kuwa na kiu ya kuona Yanga inafanya vizuri na uhakika ikitokea tunahitaji kiasi kiongezeke basi kitaongezwa, hivyo niwaombe tu mashabiki wa Yanga wakae mkao wa kula kwani Yanga inayokuja itakuwa yamoto sana,” alisema Nugaz.

 

Yanga kwa sasa ina washambuliaji halisi wanne, David Molinga, Yikpe Gnamien, Tariq Seif na Ditram Nchimbi. Tayari Yikpe yupo kwenye hatari ya kuachwa baada ya kushindwa kuonyesha uwezo.

Leave A Reply