The House of Favourite Newspapers

Yemi Alade Anusurika Katika Ajali ya Gari nchini Uhispania

0

 

Mkali aliyewahi kutikisa na Ngoma ya Johnny 2013, Yemi Alade.

MWANA-DADA anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Tasnia ya Muziki Afrika, Yemi Alade anasema amenusurika kwenye ajali ya gari alipokuwa nchini Uhispania.

Katika chapisho kwenye Instagram yake Jumanne, msanii huyo alifichua kuwa ajali hiyo ilitokea Alhamisi iliyopita akiwa safarini kati ya Barcelona na Benicassim. Hakuna vifo vilivyoripotiwa.

Alisema ajali hiyo ilitokea ghafla lakini alipata majeraha madogo.

Alade, anayejulikana kwa muziki wake wa kusisimua, alisema licha ya ajali hiyo bado alitumbuiza jukwaani saa chache baadaye siku hiyo hiyo, kisha akapata dharura ndogo ya matibabu .

Alimshukuru Mungu kufuatia shida yake, akisema “Neema yake inatosha”.

#EXCLUSIVE: MREMBO ANAEDAIWA KUTOKA na MCHEZAJI JEZI NO 10 AFUNGUKA-AWARARUA VIBAYA VIDEO VIXEN

Leave A Reply