The House of Favourite Newspapers

Yemi Alade: Natamani Penzi la Mr. Flavour

yemi-alade-kom-kom-ft-flavour-b-t-s-photo-7MWANA-DADA anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Tasnia ya Muziki Afrika, Yemi Alade hivi karibuni amefunguka kuwa anatamani sana kama mwanamuziki mwenzake na staa wa Wimbo wa Ada Ada, Mr. Flavour angekuwa mpenzi wake.

Akichonga na Kituo cha Televisheni cha Accelebrate TV, Yemi aliyewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na meneja wake Taiye Aliyu, Muigizaji Alex Ekudo na mwanamuziki mwenzake Phyno alisema Flavour ni mwanaume wa aina ya mtu anayemhitaji kuwa naye na anamvuto wa pekee.

“Natamani Flavour angeanguka kwenye mapenzi na mimi, ni mwanaume mzuri ambaye ana kila kigezo cha kumvutia mwanamke,” alisema Yemi. 

Comments are closed.