The House of Favourite Newspapers

Yondani, Kakolanya waitosa Yanga

NYOTA wa Yanga waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars nchini Lesotho, Kelvin Yondani na Beno Kakolanya, wameshindwa kusafiri na kikosi cha Yanga kilichoenda Shinyanga kucheza dhidi ya Mwadui FC ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Yanga iliyopo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 26 nyuma ya Azam na Simba, kesho itashuka kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kuumana na Mwadui iliyopo nafasi ya 13 ikiwa na alama 13.

 

Chanzo cha habari hii kimelieleza Championi Jumatano kuwa, wachezaji hao wamegoma kwenda na wenzao kwa kisingizio cha uchovu na kwamba walihitaji kupata muda wa kukaa na familia zao ambazo hawakuwa nazo kwa zaidi ya wiki tatu walipokuwa kwenye kambi ya timu ya taifa iliyokuwa Afrika Kusini.

 

“Yanga kutakuwa na tatizo kubwa ambalo viongozi wanajaribu kulificha maana ukiangalia timu imeondoka Dar leo (jana Jumanne) kwenda Shinyanga, lakini Yondani na Kakolanya wameonyesha kama kugomea safari hiyo kwa madai ya kuchoka na safari ndefu kutoka Lesotho.

 

“Mbali na Yondani na Kakolanya, pia kuna wachezaji kama Pato Ngonyani na Papy Tshishimbi nao hawajaenda wakati safu ya ulinzi inaonekana kupungukiwa watu kwani hata Abdallah Shaibu ‘Ninja’ naye yupo kwenye kikosi cha taifa chini ya miaka 23,” akilisema Chanzo hicho.

 

Baada ya Championi kupata taarifa hizo, lilimtafuta Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten ili aweze kuzungumzia jambo hilo ambapo alijibu kuwa: “Sijui ni kipi kilichowakuta Yondani na Kakolanya kiasi cha kuwafanya wasiondoke na wenzao kwani hata mimi nimesikia tu ila mwenye taarifa zaidi na hilo atakuwa Kaimu Katibu, Omari Kaya.”

Musa Mateja, Dar es Salaam.

WEMA Alivyotinga Mahakamani Tena, Kesi ya Video za Ngono!

Comments are closed.