The House of Favourite Newspapers

Young D Akubali Kumlea Mwanaye

0

MZAZI mwenza wa mkali wa Singo ya Bongo Bahati Mbaya, David Genzi `Young D,’ Mamisa amefunguka kuwa amemaliza tofauti zake na jamaa huyo baada ya kukubali kumlea mwanaye ambaye awali alidaiwa kumtelekeza.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Mamisa alisema kuwa, wameamua kumaliza tofauti zao wao wenyewe bila kumshirikisha mtu na Young D ameahidi kuwa baba bora kwa mwanaye.

“Namshukuru Mungu kwa sasa nipo sawa na mzazi mwenzangu, tuliyaongea bila kuwekwa kikao na mtu yeyote. Young D amem-chukua mtoto na anaishi na bibi yake (mama wa Young D),” alisema Mamisa.

MAYASA MARIWATA | GAZETI LA AMANI

Leave A Reply