The House of Favourite Newspapers

Young Killer: Mama ana-floo ngoma zangu zote

MKALI wa Hip Hop Bongo, Kassim Yusuph ‘Young Killer’ amefunguka kuwa mama yake mzazi ni shabiki wake namba moja na anao uwezo wa kuimba nyimbo zake zote.

 

Msanii huyo ambaye pia hupenda aitwe Msodoki aliiambia Showbiz kuwa, kitendo hicho kinamfanya azidi kumpenda mama yake huyo ambaye pia amekuwa akimpa sapoti kwenye mishe zake za kimuziki.

 

“Naweza kusema mama yangu ni shabiki wangu namba moja, ananisapoti kwa kila hali lakini pia hata nyimbo zangu zote anazi-floo fresh kabisa, ni mtu muhimu sana kwangu,” alisema Msodoki.

SHAMUMA AWADHI | IJUMAA WIKIENDA

SUPRISE ya Aslay, Beka kwenye Party ya DJ wa KIBA

Comments are closed.