YOUNG KILLER, YOUNG D KIMENUKA DAR LIVE – (VIDEO + PICHAZ)

‘MADOGO’ wakali wa Bongo Fleva, Young Killer na Yaoung D, wamekinukisha vilivyo usiku wa kuamkia leo baada ya kila mmoja wao kupiga shoo ya aina yake katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala Zakhiem na kuwaacha mashabiki wakishindwa kuamua nani zaidi kati yao wawili.

Katika shoo hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya mashabiki na wapenda burudani ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri, wasanii wote walikuwa wakitambiana huku kila mmoja akionyesha uwezo wake wa kuchana, kucheza na jukwaa na kuburudisha.

Kwa awamu tofauti, Killer na Young D walipokelewa na jukwaa kwa sahangwe, miruzi na amsha-amsha huku kila mmoja akitumia mbinu zake zote kumfika mwenzake.

Licha ya wakali hao kuweka historia ya kupanda Jukwaa moja, siku moja lakini bado walionyesha uhasimu wao bado haujamalizika.

Kwa upande wa Young Killer alidai hajamaliza uhasama ‘bifu’ na young D hadi pale atakapomuomba msamaha.

Wasanii hao wamekuwa kwenye vita ya kiburudani kwa miaka kadhaa sasa huku kila mmoja akitamba kuwa ni mbabe kuliko mwenzake.

YOUNG D Kuhusu Kumaliza Bifu na Young Killer


Loading...

Toa comment