The House of Favourite Newspapers

Yusuf Mlela akiri hana alichopata Bongo Muvi

0
Msanii Yusuph Mlela 'Angelo'
Msanii Yusuph Mlela ‘Angelo’

Stori: Imelda Mtema

HUKU kukiwa na madai ya kuporomoka kwa soko la filamu nchini, muigizaji mahiri Yusuf Mlela amekiri kuwa licha ya kufanya kazi nyingi, lakini hakuna chochote cha maana alichopata katika maisha yake ya uigizaji.

Akizungumza na Risasi Vibes, Mlela alisema katika kuhakikisha anasonga mbele, nusu ya maisha yake ameyahamishia jijini Nairobi, nchini Kenya ambapo angalau anaona mambo yake yanaweza kwenda vizuri.

“Unajua kiukweli nimeuza sura sana kwenye filamu nyingi lakini mafanikio ni kiduchu mno, sasa nimeamua kutafuta njia nyingine ya kuweza kunisogeza hatua moja kimaisha, niko Nairobi na huko nafanya tamthiliya, nahisi mambo yataenda vizuri,” alisema Mlela.

Leave A Reply