The House of Favourite Newspapers

UNYAMA! Baba Achinja Wanaye Mapacha, Mtoto Asimulia Alivyoshuhudia- Video

BWANA Respicius Diocress, mkazi wa Kijiji cha Butayaibega wilayani Bukoba mkoani Kagera anatuhumiwa kuchinja kwa panga na kuwatenganisha kichwa na kiwiliwili watoto wake wawili mapacha wa miaka minne, Deonidas Respicius na Diocress Respicius.

 

Aidha, imeelezwa baada ya kuwachinja mapacha hao wenye umri wa miaka minne Diocress alimkabidhi mwanawe mkubwa, Japhet Respicius (5) Biblia ili awaombee marehemu kisha yeye kutoroka na sasa wanakijiji wenzake wameazimia kumsaka.
 
Muonekano wa makaburi ya walipozikwa mapacha hao waliochinjwa na baba yao mzazi.
Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji hao, afisa mtendaji wa kijiji cha Butayaibega, Geofrey Deogratias alisema tukio hilo lilitokea saa saba usiku wa kuamkia, Jumapili, April 15, 2018.
 
“Nilifika eneo la tukio na kukuta miili ya watoto Devotha Nyangoma Respicius (4) na pacha mwenzake Johanes Kato Respicius (4) ikiwa imelazwa sebuleni katika nyumba ya mtuhumiwa, huku vichwa vyao vikiwa pembeni mwa miili hiyo” alisema.
“Huyu mtuhumiwa alikuwa na watoto watatu ndani ya nyumba yake, lakini mtoto mmoja Japhet Respicius (5) hakumuua na alishuhudia baba yake akifanya unyama huo kwa wadogo zake.”
 
 
Mtendaji huyo alisema baada ya kuona hali halisi alipiga simu polisi kutoa taarifa juu ya tukio hilo, ambao walifika na kuichukua miili hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
 
Alisema alipofika eneo la tukio alimkuta mtoto mkubwa akiwa nje ya nyumba akilia, na kuwaeleza kuwa baada ya baba yao kuwachinja wadogo zake alimkabidhi Biblia na kumsihi aendelee kuwaombea.
“Mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na kuelekea kusikojulikana, lakini ameendelea kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa mwenyekiti wa kijiji, mtendaji na baadhi ya wanafamilia” alisema mtendaji Deogratias.
Mtoto Japhet.
Alisema kuwa sehemu ya ujumbe huo ilisomeka: “Mwambie bibi Geogina ambaye ni bibi wa mke wangu aitwaye Kokwenda David kuwa nimekwishatekeleza alichokitaka kwa kuwaua Nyangoma na Kato, na mimi niko salama ila bado nawatafuta wengine wawili ili niwaue na kujipeleka polisi mwenyewe, msinitafute.”
Alisema baada ya polisi kuchukua miili ya marehemu hao, mtuhumiwa alirudi tena eneo la tukio akiwa na panga mkononi na kufyeka migomba yake na kuchoma nyumba yake moto, huku akiwatishia ndugu na jamaa zake kuwa wakimsogelea atawafyeka, na baadae alikimbia.

Taarifa zinaeleza kuwa kabla ya tukio, mtuhumiwa allikuwa akiishi na watoto wake watatu ambao mapacha hao aliwazaa na mama anaejulikana kwa jina la Deovitha David ambae kwa sasa wamekwisha achana na kubaki kama mzazi mwenzake.

 

Duru zinazidi kueleza kuwa marehemu hao mapacha kabla ya mauti kuwafika, mama yao alimuomba mzazi mwenzake kuja kuwachukua wanae wakamtembelee na kisha atawarejesha, mtuhumiwa alimkubalia mzazi mwenzake na kumtaka awarejeshe watoto hao Jumamosi ya tarehe 15 April, na baada ya mapacha hao kuwa wamerejeshwa, mama huyo aliondoka zake ambapo tukio la la mauaji hayo lilifanyika usiku huo wakati mama huyo akiwa tayari amekwisha rejea katika mji wake.

 

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambae pia ni mtoto mdogo wa kumzaa, Japhet Respicius (5) alisema usiku wa tukio baba yake mzazi aliwachukua marehemu hao kwa zamu na kisha kutelekeza mauaji hayo, na alipojaribu kuhoji walipo ndugu zake alimjibu kuwa wapo mbinguni.

 

 

Mtoto ndiye alikuwa wa kwanza kutoa taarifa kwa ndugu jamaa na majirani ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa kijiji Bulambuzi.

 

Kisa kamili cha mauaji hayo mpaka sasa hakijajulikana japo inahusishwa na mgogoro wa kimapenzi uliokuwa ukiendelea kati ya wanandoa haona wengine wakihusisha na kile walichokiita wivu wa mapenzi. Juhudi za kutaka kuhahamu ukweli kutoka mama wa marehemu zimeshindikana mpaka sasa kutokana na majonzi na huzuni mkubwa uliopelekea mama huyo kushindwa kabisa kuongea na vyombo vya habari.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema baada ya msako mkali, mtuhumiwa ametiwa mbaroni  jana Aprili 16  jijini Mwanza baada ya kutoroka na taratibu za kumsafirisha ili akabiliane na mashitaka zinafanyika.

UNYAMA WA KUTISHA! Baba Achinja Wanaye Mapacha, Mtoto Asimulia!

MAFURIKO DAR

Comments are closed.