The House of Favourite Newspapers

Diamond Mbaroni Kwa Kusambaza Picha Chafu, Nandy Asakwa – Video

Mwanamuziki nyota, Diamond Platinumz.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema kuna baadhi ya wasanii ambao walianza kufanya uhuni ndani ya mitandao akiwemo mwanamuziki nyota, Diamond Platinumz, ambaye tayari amekamatwa na polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha.

 

Mwakyembe ameliagiza Jeshi la Polisi kumsaka msanii, Nandy ili naye ahojiwe kutokana na tuhuma kama hizo ambapo yeye video yake na Bil Nas ilisambaa mitandaoni wakijiachia kimahaba.

 

Mwakyembe amesema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyehoji akitaka kujua serikali ina mkakati gani kutokana na wimbi la wasanii kuachia video na picha zao utupu mitandaoni.

 

Aidha, Mwakyembe alisema Tanzania siyo kokoro la uchafu na kueleza kwamba wanaangalia taratibu za kuwafikisha Diamond na Nandy mahakamani kutokana na tuhuma hizo.

 

VIDEO: MSIKIE MWAKYEMBE AKINENA

VIDEO: MSIKIE MWAKYEMBE AKINENA

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe.
 

Diamond na Nandy wahojiwa polisi kisa video chafu.

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on


Pia Mwakyembe amesema imebidi mwanamuziki Faustina Charles ‘Nandy’ naye akamatwe kisha kuhojiwa na wanaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani.

Mwakyembe ametoa wito kwa vijana kuwa mitandao si kokoro la kupeleka uchafu wote ambao umezuiwa na sheria na kwamba nchi ina utamaduni wake ambapo inahitajika kulinda kizazi cha sasa na cha kesho.

 

Diamond na Nandy wahojiwa polisi kisa video chafu.

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Comments are closed.