visa

Zahera Amuacha Kiungo Yanga

AKIWA na uhakika wa safari ya Botswana, kiungo mshambuliaji, Jaffer Mohamed ‘rasta’ juzi alikatwa dakika za mwisho na kuwekwa mshambuliaji raia wa Kenya, Maybin Kalengo.

 

Awali, kiungo alikuwepo kwenye orodha ya wachezaji 21 waliotarajiwa kusafi ri kuelekea nchini huko kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo.

 

Timu hiyo tayari ipo Botswana ambapo Jumamosi hii itacheza na Township Rollers, Gaborone, Botswana. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, kiungo huyo alikuwepo kwenye mipango ya safari baadaye kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera alimuondoa.

 

Chanzo kilisema uongozi ulipokea majina ya awali ya wachezaji watakaosafiri likiwemo jina la Jaffer ambalo baada ya muda mchache walipokea simu ya kocha akiomba aondolewe na Kalengo achukue nafasi yake.

Championi Jumatano lilipomtafuta Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema: “Tulipokea simu ya kocha akitaka Jaff er aachwe nafasi yake achukue Kalengo, uongozi hatuwezi kuingilia masuala ya kiufundi, yeye ndiye anayejua mchezaji gani anamuhitaji kwa wakati sahihi, tunaheshimu mipango ya kocha kwa kumuondoa Jaff er na kumuingiza Kalengo,”.

 

Msafara wa Yanga uliosafi ri juzi kuelekea Botswana ni Metacha Mnata, Paulo Godff rey, Kelvin Yondani, Muharami Issa ‘Marcelo’, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro, Papy Tshishimbi, Mapinduzi Balama, Mohamed Issa. Wengine Ramadhani Kabwili, Sydney Khoetage, Rafael Daudi, Juma Balinya, Patrick Sibomana, Ally Ally, Feisal Salum, Issa Brigimana, Deus Kaseke, Mrisho Ngasa na Kalengo.
Toa comment