Kigogo walipa Betika heshima yake

WASOMAJI wa Gazeti la BETIKA maeneo ya Kigogo Sambusa jijini Dar es Salaam, wamesema kuwa, wamekuwa wakilifuatilia gazeti hilo, hivyo linastahili kupongezwa.

 

Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, linatolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na huingia mtaani kila Jumatano.

 

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, pia lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Leo Jumatano, timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, ilitembelea maeneo hayo na kukutana na wasomaji mbalimbali wa Gazeti la Betika.

Idrissa Mohamed ambaye ni mmoja wa wasomaji wa gazeti hilo, alisema Betika limekuwa bora siku hadi siku tangu liingie mtaani.

 

“Tunashukuru kwa leo kututembelea, kiukweli Gazeti la Betika hapa kwetu tunalifahamu vizuri sana kwani tunalifuatilia tangu lilipoingia mtaani.

 

“Linasaidia sana katika haya masuala ya kubeti, hivyo niwapongeze kwa kutuletea kitu kama hiki,” alisema.

Naye Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema heshima ya Betika imeendelea kukua kila siku na sasa wanajivunia kuwa na idadi kubwa ya makampuni yanayotangaza biashara zao kupitia gazeti hilo hasa kwa kuwa bei yao ni nafuu na imewavutia wengi, huku akiongeza kuwa bado wanawakaribisha watu binafsi na makampuni kuleta matangazo yao.

“Hili ni gazeti la bure, linawahusu watu wazima kuanzia umri wa miaka 18, linatolewa bure kabisa kwa wauza magazeti wote nchini.

 

“Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao yetu ya kijamii katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

 

“Kupitia hayo matangazo ambayo yapo ndani ya Betika, msomaji akijipatia nakala yake anapata faida mara mbili, kwanza kufahamu odds mbalimbali za kubet, lakini pia kufahamu mambo mbalimbali yanayowahusu watangazaji wetu hao.

“Wanaohitaji kutangaza nasi tunapatikana kupitia namba 0755826488 na 0712595636 au barua pepe [email protected], bei zetu ni nafuu, muhusika anaweza kufika Sinza Mori, Dar, kwenye jengo letu la Global Group,” alisema.


Toa comment