The House of Favourite Newspapers

Zahera Arejea Na Usajili Mpya Yanga

Mwinyi Zahera.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amepanga akirejea tu nchini kutoka kwao, moja kwa moja atakutana na Kamati ya Usajili ya Yanga ili kujadiliana juu ya usajili wa dirisha dogo.

 

Zahera raia wa DR Congo, jana Jumanne aliiongoza timu yake hiyo ya taifa kucheza na Zimbabwe kwenye mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).

 

Baada ya kumaliza majukumu yake ya timu ya taifa, kocha huyo anatarajiwa kurejea Tanzania muda wowote kuendelea na majukumu ya klabu ikiwa wikiendi hii timu yake ya Yanga ina kibarua cha kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Alliance kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Zahera katika usajili wa dirisha dogo, amepanga kushusha vifaa vitatu kutoka DR Congo ambapo ni washambuliaji wawili na kiungo mmoja.

 

“Nikirudi tu nitakutana na viongozi wangu wa juu kwa ajili ya kujadili kuhusu usajili wa dirisha dogo, hasa wale wachezaji ambao nimewapendekeza, baada ya hapo ndipo mambo mengine yatafuata.

 

“Nataka niimarishe zaidi timu yangu ili iweze kupambana vizuri katika ligi na mashindano mengine, hivyo ni lazima tufanye usajili makini,” alisema Zahera

Comments are closed.