The House of Favourite Newspapers

Zaidi ya Mil 100 Zatengwa Kuibua Vipaji vya Michezo Same

Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Dkt. Mathayo David Mathayo akizungumza na wananchi wa jimbo lake katika ziara yake ya kikazi.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao wakati akiwahutubia.

 

 

Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Dkt. Mathayo David Mathayo ametenga zaidi ya shilingi million mia moja kwa ajili ya kuibua vipaji na kuimarisha michezo katika jimbo hilo.

 

Mbunge huyo ambaye ameanza kugawa mipira katika kila kata kwa ajili ya maandalizi ya mashinda hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao yatashindanisha timu za wanawake kwa upande wa mpira wa pete na wanaume kwa upande wa mpira wa miguu.

 

Akizungumza na wananchi wa kata zote 20 anazotembelea Mathayo amesema katika kila kata watashindana vijiji kwa vijiji kwa mtindo wa marudiano mara tatu tatu ili aweze kupatikana mshindi kwa upande wa wanawake na wanaume.

 

“Nataka mshindane kila kijiji na kijiji na kitakachoshinda kwenye kila kata, kitapata zawadi ya shilingi milioni mbili kwa timu ya wanawake na shilingi milioni mbili kwa timu ya wanaume”alisema Mathayo.

 

Mathayo amesema ametenga shilingi milioni themanini taslim kwa ajili ya timu zitakazoibuka  kidedea katika kila kata.

 

“Ndugu zangu michezo ni afya michezo ni ajira leo namkabidhi diwani wenu hii mipira lakini asiigawe mpaka nitakapoleta jezi ili muanze mashindano hayo mkiwa na jezi zinazotofautina au mnataka kucheza kienyeji?”alihoji Mathayo.

 

Mathayo pia amekuwa akigawa mipira katika shule za msingi na sekondari katika kata mbalimbali jimboni kwake ikiwa na lengo la kuimarisha michezo shuleni. .

Comments are closed.