The House of Favourite Newspapers

Zanzibar Heroes Kurudia Maajabu Fainali Ya Chalenji Dhidi Kenya Leo

Mchezo ukiendelea.

ZANZIBAR Heroes leo Jumapili inacheza fainali ya kombe la chalenji dhidi ya mwenyeji Kenya kwenye Uwanja wenye miundo mbinu ya kisasa wa Machakos, Kenya.

 

Heroes wanajivunia rekodi ya kucheza na wenyeji Uganda katika fainali ya mwaka 1995 jijini Kampala na kumfunga mwenyeji bao 1-0 mbele ya utitiri wa mashabiki.

 

Kocha wa Heroes ambayo iliwapiga Uganda mabao 2-1 na kufuzu kwenye hatua hiyo, Hemed Morocco amesema atahakikisha wanacheza kufa na kupona kulinda heshima ya Tanzania.

Kikosi cha timu ya ZANZIBAR Heroes

Heroes imeweka rekodi ya kipekee katika michezo mitano ambayo imecheza kwani imetoa wachezaji bora wanne ambao ni Feisal Salum dhidi ya Kenya, Mohamed Issa dhidi ya Rwanda, Ibrahim Hamada dhidi Kilimanjaro Stars na Abdulaziz Makame dhidi ya Uganda.

 

Morocco ameiambia Spoti Xtra kwamba; “Si mechi rahisi kama wengi wanavyofikiria lakini kwa upande wetu tutapambana kufa kupona kuhakikisha tunaleta kombe nyumbani kutokana na maandalizi tuliyofanya na wachezaji wangu wanahamasa kubwa.”

 

ìKikubwa tunaomba sapoti kutoka kwa Watanzania wetu wazidi kutuombea tuweze kufanya vyema kwenye mchezo huu na kuandika historia mwaka huu,î alisema Morocco ambaye ameivia chini ya makocha wakubwa akiwemo Marcio Maximo.

STORI MARTHA MBOMA

Comments are closed.